• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Sunday, October 28, 2012

    LIL WAYNE ALAZWA HOSPITAL MARAMBILI NDANI YA SAA 24.

    NEWZ>>>FILEX MMARI





    Rapper lil wayne amelazwa tena hospitali baada ya kupata tatizo lingine linalofanana na alilolipata akiwa kwenye ndege binafsi.
    Mwanzilishi huyo wa Young Money Entertainment alikuwa amesharuhusiwa kutoka hospitali jana kutokana na kupatwa na dalili za kifafa.
    Weezy alikuwa kwenye ndege akitokea Texas kuelekea Los angeles wakati tukio la pili li
    lipotokea baada ya kuanza tena safari iliyokuwa imekatishwa kwa muda.
    Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa weezy alilazwa kwa mara ya pili kwenye hospitali iliyopo Louisiana.
    Juzi Lil wayne alipelekwa kwenye hospitali ya huko Texas baada ya kupatwa dalili hizo akiwa kwenye private jet kiasi cha kumfanya atue kwa dharura.
    Lil wayne a.k.a Dwayne Carter Jr yupo busy na maandalizi ya album yake mpya "Am not a human being 2" itakayotoka december.
    Pia ameandika kitabu cha historia ya kiitwacho "Gone till november" kinachohusiana na miezi nane aliyokaa kwenye gereza la Rickers island kwa kosa la kumiliki silaha.

    No comments:

    3500K