• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, October 22, 2012

    Kufuru:Wema Sepetu Amuogesha Mrembo kwa Pombe Kali




    KATIKA kuonesha jeuri ya fedha, Wema Isaac Sepetu amefanya kufuru kama kawaida yake baada ya kumlowanisha mwili mzima kwa pombe za bei mbaya mrembo aitwaye Rehema Kimbu.

    Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri nyumbani kwa mwigizaji Aunt Ezekiel, Mwananyamala, Dar, Ijumaa iliyopita ambapo Wema na Aunt walimfanyia ‘sapraizi’ ya birthday  Rehema ambaye ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

    Katika hali ya kushangaza, Rehema ambaye ni shosti mkubwa wa Aunt alishtukia anamwagiwa pombe mfululizo aina ya Gordon’s na Jack Daniels huku mwigizaji Nice Chande akimmiminia chupa kubwa kadhaa za maji.

    Muda mwingi Wema alikuwa akimmwagia Rehema pombe bila kushusha mkono. Kufuatia kitendo hicho kilichoambatana na kelele nyingi za mastaa hao,  kilisababisha wapita njia kujazana getini kwa Aunt bila kujua kilichokuwa kikiendelea na kudhani Rehema alikuwa akipokea kipigo. chanzo udaku blog

    No comments:

    3500K