Wakati wasomi wengi wakisisitiza kuhusu vijana kutambua umuhimu wa
elimu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond' amedai
kuwa anatamani kurudi shule kuendelea na masomo lakini kutokana na shughuli zake za muziki anakosa nafasi.
Akiongea alidai kuwa anaamini elimu yake ya kidato cha nne ni ndogo sana na ana changamoto nyingi ili kufikia level za kimataifa, hivyo ana mipango ya kurudi shule lakini akifikilia mambo mengi muziki na ratiba za show huwa anakata tamaa kabisa lakini anaamini atafanya hivyo siku moja ili kutimiza ndoto yake ya kufika mbali zaidi kielimu.
Diamond alisema kuwa kuna umuhimu wa yeye kwenda shule lakini kwa sasa hafikirii kama anaweza kukaa darasani tena na kumsikiliza mwalimu pengine aende nje kwa ajili ya kusomea muziki huku akiendelea na kazi hiyo hata huko atakapokuwa akisoma.
"Naweza kurudi shule lakini pengine nikasomee muziki na mambo mengine yanayohusu muziki" Alisema Diamond.

No comments:
Post a Comment