• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, September 10, 2012

    TANZANIA SOCIAL NEWS: MTOTO AUAWA ACHUNWA NGOZI

    MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Nyarigamba iliyoko Kata ya Muhutwe wilayani Muleba, mkoani Kagera, Beatha James (12), ameuawa kikatili na kisha kunyofolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili na kung’olewa meno.
    Mwili wa marehemu ambao ulipatikana baada ya siku nane maeneo ya kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya, ulikutwa umechunwa ngozi, shingo imekatwa, ulimi umetolewa, meno yameng’olewa, sehemu zake za siri zikiwa zimeondolewa na kunyolewa nywele huku akiwa na matundu kichwani. Kwa mujibu wa maelezo ya mama mkubwa wa marehemu, Eyudosia  Salvatory, aliyekuwa akiishi naye katika Kitongoji cha Bitende, mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani Agosti 29 mwaka huu majira ya saa 3.30 asubuhi akielekea kwa mama yake mdogo mwingine aitwaye Mariagoleti Ishengoma.Eyudosia amesema baada ya kufika huko alitumwa akafuate maziwa kwa jirani yao aitwaye Erasmo Sostenes, lakini akatumia muda mrefu bila kurejea ndipo walipopiga simu sehemu wanayochukua maziwa  wakaambiwa kuwa hajafika na maziwa bado hayajachukuliwa. Na kuongeza kwamba  Septemba 7 mwaka huu, ndipo walipopata taarifa za kupatikana maiti ya mtoto huyo katika maeneo ya Kaboya karibu na kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Taarifa za mwili huo zilitolewa na wawindaji wanaowinda wanyama waharibifu na kuwa walipofika walikuta mwili wa Beatha ukiwa umechunwa ngozi, shingo imekatwa, ulimi umetolewa, meno yameng’olewa, sehemu zake za siri zikiwa zimeondolewa na kunyofolewa nywele huku akiwa na matundu kichwani, huku sura ilikuwa imeharibika hivyo waliweza kumtambua kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa kabla ya kukutwa na mauti. Mtendaji wa kijiji hicho, Dominic Damasenyi, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa zilitolewa kwake na wanafamilia.

    No comments:

    3500K