• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, September 10, 2012

    MIDDLE EAST NEWS: MAKAMU WA RAIS AHUKUMIWA KIFO

    Mahakama moja ya Iraq imewahukumu adhabu ya kifo Tariq al Hashimi Makamu wa Rais wa nchi hiyo aliyeikimbia nchi na msaidizi wake kwa kuhusika katika vitendo vya kigaidi na kuendesha kikosi cha mauaji. 
    Hashimi anatuhumiwa kuhusika katika mashambulizi ya mabomu dhidi ya serikali na maafisa wa usalama wa nchi hiyo miaka kadhaa iliyopita likiwemo shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari lililotekelezwa mwezi Novemba mwaka jana huko Baghdad mji mkuu wa Iraq ambalo lilikuwa limekusudia kumlenga Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Tarehe 19 Disemba mwaka jana kamati ya uchunguzi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ilitoa waranti wa kumtia mbaroni Tariq al Hashimi baada ya walinzi wake watatu kukiri kuwa walikuwa wakiamuriwa na Makamu huyo wa Rais wa Iraq kutekeleza mashambulio ya kigaidi. Hata hivyo al Hashimi baadae alikimbilia huko Kurdistan.

    No comments:

    3500K