• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, September 3, 2012

    ASIA POLITICAL NEWS: MAREKANI YASHAMBULIA NA KUUA 13 YEMEN

    Ndege za kijeshi zisizo na rubani za Marekani zimetekeleza shambulio nchini Yemen na kuua watu wasiopungua 13.
    Hayo yamethibitishwa na kingozi mmoja wa ngazi za juu wa Yemen ambaye hakutaka jina lake litajwe  na kuongeza kuwa, shambulio hilo lililofanywa na ndege za Marekani zisizo na rubani, lilifanyika hapo jana dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa na mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida. Amesema kuwa, shambulio hilo halikuweza kupiga eneo husika na badala yake lililenga magari mawili ya raia katika mji wa Radda unaopatikana katika mkoa wa Al Bayda ambapo watu 13 waliuawa papo hapo wakiwemo wanawake wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya. Wananchi wa Yemen wamekuwa wakipinga vikali uingiliaji wa Marekani nchi mwao sambamba na kufanya maandamano makubwa huku wakitoa nara za "Mauti kwa Marekani, Mauti kwa Israel." Mbali na Wayemeni hao kupinga uingiliaji wa Marekani nchini kwao, wanapinga na kulaani mashambulizi ya ndege hizo zisizo na Rubani nchini humo ambayo mwezi uliopita yaliua idadi kubwa ya raia wasio na hatia. Hivi karibuni Rais Barack Obama wa Marekani alijigamba akidai kuwa, kila Mmarekani anaona fakhari kwamba nchini yake ina nguvu na inaheshimiwa kwa kuendesha vitani zaidi duniani.

    No comments:

    3500K