• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, August 28, 2012

    TANZANIA POLITICAL NEWS: KESI YA MTIKILA YAPIGWA KALENDA HADI SEPTEMBA 6

    HUKUMU ya kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila,  imekwama na badala yake  sasa itatolewa Septemba 6 mwaka huu.

    Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika  maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.  Hukumu hiyo ilitarajiwa kusomwa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ilvin Mugeta anayesikiliza kesi hiyo. Kutosomwa kwa hukumu hiyo,  kumetokana na Hakimu Mugeta na wakili wa Serikali ambaye amaekuwa akiendesha kesi hiyo kutokuwapo mahakamani.  Akiahirisha hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Frank Moshi amesema Hakimu Mugeta alikuwa na majukumu mengine nje ya ofisi na kwamba amependekeza kuisoma hukumu  Septemba 6 mwaka huu.  Upande wa mashtaka katika kesi hiyo unadai kuwa  Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi kuwa ‘Papa alikuwa na mgeni ambaye ni gaidi, ninaomba niseme haya kwa sababu ninasema mimi, Rais Kikwete ni gaidi. "He is a terrorist ".  Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Mtikila pia alitoa maneno mengine ya uchochezi, na chuki na dharau na yangeweza kusababisha watu kukosa imani kwa Serikali yao.  Imedaiwa kuwa maeneo hayo ni pamoja na kusema  “uteuzi wa Jakaya Kikwete siku zote unaongozwa na imani yake ya dini kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi....''  Hata hivyo Mtikila amekana mashtaka yotena katika utetezi wake, alidai kuwa angewaita mahakamani mashahidi 10.  Hata hivyo alimuita shahidi mmoja, aliyekuwa Mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya Mwananchi Communications, Mpoki  Bukuku.

    No comments:

    3500K