• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, August 29, 2012

    Post titleHABARI KUTOKA MBEYA POLISI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA HADHARA



    JESHI la Polisi Mkoani Mbeya limesema halitaruhusu mikusanyiko ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa wakati zoezi la sensa ya kuhesabu watu na makazi linaloendelea mkoani hapa na kuwa chama chochote cha siasa kitakacho kiuka agizo hilo hatua kali za  sheria zitachukua mkondo wake.
    Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Diwan Athuman wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana na na baadhi ya vyama vya siasa kuendesha mikutano katika maeneo mengine hapa nchini. Kamanda Diwani amesema kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kuendesha mikutano ya kisiasa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini wakati zoezi la sensa likiendelea inaweza kuathili mwenendo mzima wa zoezi hilo ambalo linamanufaa kwa watanzania wote. Aidha amesema kuna baadhi ya wanasiasa ambao wamekwenda katika ofisi yake kwa lengo la kuomba kibali cha mikutano ya kisiasa,ambapo amejitahidi  kuwaelewesha juu ya umhimu wa zoezi hilo kwa masrahi ya taifa. Hata hivyo  Diwani amesema jeshi la polisi halipo tayari kuwafumbia macho wanasiasa ambao watakiuka utaratibu huo ambao unalenga kulinda zoezi hilo la sensa kutoathiliwa na mikutano hiyo ya hadhara ambayo inaweza kuchochea vulugu miongoni mwa wananchi kwa kushindwa kuhesabiwa ipasavyo. Pia ameongeza kuwa kitendo hicho kitaharibu utaratibu wa serikali wa kufanikisha zoezi la kupata takwimu sahihi kwa kila mtanzania kwa ajili ya kuiwezesha serikali kupanga mipango ya miradi ya maendeleo ya wananchi ambayo itakuwa na iwiano uliosawa. Kamanda huyo amebaishisha kuwa mpaka sasa zoezi la kuhesabu watu na makazi linaendelea vizuri mkoani hapa kwa kuwa hakuna malalamiko yoyote jitokeza na kuwa jeshi hilo limeimarisha ulinzi wa kutosha kwa maeneo yote mkoani humo. Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya kwa  sharti la kutokutajwa majina ,wamekasirishwa na kitendo cha baadhi ya wanasiasa kuendesha mikutano ya hadhara kwa baadhi ya mikoa ambayo inachochea na kuleta vulugu wakati zoezi la sensa likiendelea kwa nchi nzima. Wamesema zoezi la sensa ni la manufaa kwa watanzania wote bila ya kujali  itikadi za siasa na dini kwa kuwa linaiwezesha serikali iliyopo madarakani kutekeleza malengo yake kwa ufanisi.

    No comments:

    3500K