• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Friday, August 31, 2012

    TANZANIA POLITICAL NEWS: DK. SLAA KUMJIBU SAMUEL SITTA

    KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema kauli iliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni nzito, hivyo anajipanga kuijibu.
    Dk Slaa amesema asingependa kuzungumzia kauli hiyo sasa kwa kuwa yuko ziarani vijijini, lakini ataitolea tamko wakati mwafaka ukifika. Habari ambazo Dk Slaa mwenyewe jana jioni amethibitisha kwamba atakutana na waandishi wa habari leo mjini Iringa, lakini hakuwa tayari kueleza kama atazungumzia kauli ya Sitta au la. Kauli ya Dk Slaa imekuja baada ya vyombo vya habari nchini kumtaka azungumzie kauli ya Sitta kuwa muda wa Chadema kutawala nchi bado, kwa kuwa chama hicho hakina viongozi makini wa kufanya kazi za Serikali. Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene  amesema mkutano wa Dk Slaa na waandishi wa habari utalenga kueleza jinsi Chadema kinavyoendesha Operesheni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), baada ya kuzuiwa kwa mikutano yake ya hadhara. Sitta alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM wa wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera juzi, alisema kuna upungufu mwingi katika safu ya uongozi ya Chadema, kutokana na kutokuwa na watu wenye uzoefu wa kufanya kazi za Serikali, badala yake wana baadhi ya watu wenye uzoefu wa kuongoza kumbi za muziki. Sitta amesema ukimwondoa Dk Slaa, hakuna kiongozi mwingine anayeweza kufanya kazi ya kukiongoza na kukifanya chama hicho kikubalike kwa umma.

    No comments:

    3500K