• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, August 15, 2012

    MESSI, RONALDO NA INIESTA KUGOMBEA TUZO YA MCHEZAJI BORA UEFA.



    MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo, nyota wa Barcelona Lionel Messi na Andres Iniesta wamechaguliwa kugombea tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani
    humo-UEFA. Majina hayo matatu ya wachezaji hao ndio majina yaliyopata kura nyingi zaidi kati ya kura 53 za waandishi wa habari za michezo wanaowakilisha vyama vya soka vya nchi zao ambazo ni wanachama wa UEFA. Katika kura hizo kiungo wa klabu ya Juventus, Andrea Pirlo alishika nafasi ya nne wakati Xavi Hernandez wa Barcelona ambaye alimaliza katika nafasi ya pili katika tuzo za mwaka jana alishika nafasi ya tano. Wachezaji hao watatu walioingia katika orodha ya tatu bora wataenda jijini Monaco wakati wa shughuli za upangaji ratiba ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo na mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa kutokana na kura zilizopigwa Agosti 30 mwaka huu.

    No comments:

    3500K