Waasi wanaopigana kuuondoa madarakani
utawala wa Rais Bashar al Assad wa Syria kwa mara ya kwanza wamepata silaha za
mizinga ya kurushwa kutokea angani.
Kituo
cha televisheni cha NBS kimeripoti kuwa Jeshi Huru la Waasi wa Syria, FSA,
limepata kiasi kidogo cha silaha hizo ambazo ziliwafikia kupitia jirani yao
Uturuki ambayo imekuwa ikimtaka Rais Assad aachie ngazi kufuatia wimbi la
mauwaji. Maafisa wa Marekani walisema hapo awali kuwa nchi jirani na Syria
zinazotaka utawala wa Assad uondoke ikiwemo Saudi Arabia na Qatar zinashinikiza
waasi wapewe silaha za aina hiyo. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na
ongezeko la mashambulizi ya angani kutoka kwa vikosi vya serikali hasa kwenye
mji wa Aleppo, na kuwafanya waasi kuhitaji silaha hizo kwa dharura.
Hata hivyo
NBS haikutaja ni aina gani ya silaha hizo zijulikanazo kama MANPADs wamepewa
waasi hao. Kwa kawaida zipo za teknolojia ya chini hadi za hali ya juu.
No comments:
Post a Comment