• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Friday, August 31, 2012

    AFRICA POLITICAL NEWS: ANGOLA UCHAGUZI LEO

    Kampeni za uchaguzi zimemalizika nchini Angola huku wananchi wakitarajiwa kushiriki uchaguzi wa bunge hii leo Ijumaa, majira ya saa moja kwa saa za Angola.
    Ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya chama tawala MPLA na kile cha upinzani UNITA. Hata hivyo, wachambuzi wa kisiasa wanatabiri kuwa chama tawala huenda kikajipatia ushindi mkubwa kutokana na serikali ya Rais Edwardo Dos Santos kutumia raslimali nyingi za serikali kwenye kampeni zake. Wakati huo huo kiongozi wa chama cha UNITA, Isaias Samakuva amedai kuwa maisha yake yako hatarini. Duru za karibu na mwanasiasa huyo zinasema kuwa, mtu mwenye silaha alikamatwa juzi katika mkutano wa kisiasa alipokuwa akimkaribia Bw. Samakuva. Serikali imekanusha kuhusika na tukio hilo na imeahidi kumuongezea ulinzi mkuu huyo wa upinzani.

    No comments:

    3500K