• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, July 5, 2012

    Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka, Rafiki yake atoa ushuhuda mpya jinsi alivyo tekwa






    TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI, RAFIKI YAKE ATOA USHUHUDA MPYA WA JINSI ALIVYOTEKWA
    Waandishi wetu
    WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika hospitali moja ya huko Ujerumani.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu yake sasa.


    Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.


    “Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
    Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”


    Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.


    Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”

    “Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”


    Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alipoulizwa juu ya suala hilo alipinga na kusema; “Habari za aina hiyo mtakuwa mnazipata nyingi, najua  mtaandika, ndiyo maana mnaandika madaktari Muhimbili wanafanya kazi wakati si kweli”.


    Alisisitiza kuwa Dk Ulimboka yupo Afrika Kusini  anakopatiwa matibabu na kusisitiza kuwa habari alizokuwa nazo tangu juzi jioni ni kwamba anaendelea vizuri.


    Katibu wa Chama cha Taifa cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa juu ya hali ya Dk Ulimboka alisema kwa mujibu wa taarifa za juzi jioni alikuwa anaendelea vizuri.


    Alipoulizwa juu ya taarifa za kupelekwa Ujerumani aliguna kisha akasema: “Naomba ieleweke kuwa yupo Afrika ya Kusini kwa matibabu.


    Rafiki asimulia mkasa


    Rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka aliyekuwa naye wakati mkasa wa kutekwa ukitokea, Dk. Deogratius Michael ameelezea tukio zima lilivyotokea na kusema ulikuwa wa kitaalamu na ulifanywa na watu wenye ujuzi na mambo hayo.

    No comments:

    3500K