Atapambana na bondia kutoka Uganda kugombea mkanda wa
IBF Afrika
■ Mpambano huo wa kukata na shoka
utafanyika siku ya Idd pili
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF
limetangaza rasmi mpambano kati ya bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania na Sande Kizito kutoka Uganda.
Mpambano huo utafanyika kutafuta bingwa wa “IBF Continental Afrika” katika uzito wa Unyoya
(Featherweight) kilo 58 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-Es-Salaam.
Bondia Ramadhani Shauri anatoka katika kundi la kocha Mzazi
lenye makao yake makuu Ubongo katika eneo la Mabibo. Shauri ana rekodi ya
mapabano 12 ambapo katika maisha yake ya ngumi ameshinda mara 11na kupoteza
mara 1. Naye bondia Sande Kizito ana rekodi ya mapambano 12 ambapo ameshinda
mapamambano 7 na kupoteza 9.
Aidha, bondia Nasibu Ramadhani atapambana na
bondia Twalibu Mubiru toka Kenya
kugombea mkanda wa “IBF East & Central Africa” katika
uzito wa Bantam. Nassibu Ramadhani ana rekodi ya mapambano 9 na
kupoteza mara 2 wakati Twalib Mubiru ana rekodi ya mapambano 11 amepoteza mara
7 na kutoka draw mara 2.
Mpambano kati ya Ramadhani Shauri na Sande Kizito
unafanyika wakati Tanzania
ikijijenga katika medani ya michezo ya kimataifa. Tayari Rais Jakaye Mrisho
Kikwete ameshakutana na viongozi wa vyama na taasisi mbalimbali za michezo
kujadili programu za kuiendeleza michezo hapa Tanzania.
Promota wa mpambano huo mkubwa uliopewa jina la “The
Rumble in the City” ni mfanyabiashara maarufu katika jiji la
Dar-Es-Salaam Lucas Rutainurwa wa kampuni maarufu ya Kitwe General
Traders ya jijini Dar-Es-Salaam.
Kampuni hii ndiyo iliyopromoti mpambano mwingine wa IBF
mwezi wa Aprili ambapo ulimshughudia bondia machachari wa Tanzania anayejiita kuwa mbunge wa Rorya kwa
wakazi wa jimbo hilo
wanaoishi katika jijini Dar-Es-Salaam Manda Maugo akipoteza katika raundi
ya nane!
Nalo Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lilizindua
program maalum ya “Utalii wa Michezo” katika mkutano wake wa
29 uliofanyika mwezi wa Juni uliofanyika katika jijini la Honolulu jimbo la
Hawaii nchini Marekani ambayo imelenga kuinua mchezo wa ngumi katika bara la
Afrika wakati nchi za Ghana na Tanzania ni nchi za mfano (Pilot Countries).
Katika programu hii ya “Utalii wa MIchezo” IBF
mbali na kuwapa nafasi mabondia kadhaa toka Tanzania
na Ghana kugombea mikanda mbalimbali
itaendesha pia programu ya mikutano yake hapa Tanzania na kuwaleta wanachama wake
kupanda wa mlima Kilimanjaro kila mwaka. Programu hii itawaleta watalii wengi
nchini Tanzania
na kutangaza vivutio vya kitalii kupitia michezo.
Tayari bondia Helen Joseph wa Ghana
anategemea kupanda ulingoni Agosti 11 kupambana na bondia Dahianna Santana
wa Dominican Republic
kugombea mkanda wa dunia katika uzito wa unyoya (Featherweight) upande wa
wanawake. Mpambano huo utafanyika wiki mbili kabla ya mpambano wa Ramadhani
Shauri ya Sande Kizito.
Wakati huo huo promota wa mpambano huo bwaan Lucas
Rutainurwa akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa ameamua kuwekeza
katika “Utalii wa Michezo” ili kuwawezesha vijana kujiajiri na
kujenga uchumi wa nchi ya Tanzania.
Rutainurwa alisema kuwa ana ratiba ya
mapambano ya ubingwa wa Afrika kila baada ya miezi miwili mwaka huu na mwak
akesho ambayo itaipa Tanzania
nafasi ya kunyanyua medani ya michezo pamoja na kuwawezesha vijana kujiajiri.
Ameziomba kampuni pamoja na watu wenye mapenzi mema
kujitokeza kwa wingi kusaidia kufadhili mapamnano haya ili kuiwezesha Tanzania
kuinuka kimichezo.
No comments:
Post a Comment