• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, July 5, 2012

    STEVE NYERERE AKABIDHI FILAMU YAKE YA MWL NYERERE KWA MAMA MARIA NYERERE


    Mwigizaji wa filamu nchini Stive Mangele 'Stive Nyerere jana alikuwa anakabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa  Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama. Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake  katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.

    Mama Maria Nyerere akionyesha filamu hizo alizokabidhiwa na Steve Nyerere
     
    Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda, na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake. Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ili ikamilika.

    No comments:

    3500K