Mbunge wa
Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akimpongeza Dr. Asha Rose Migiro kwa
kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa walipokutana leo katika Uwanja wa ndege.
Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini
Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati akirejea
nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
nchini Hoyce Temu.
Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga
kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.
Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro
ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Benard Membe (gari la
pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.
Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa
shangwe na zawadi za maua kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na
wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.
Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na
baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto
ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiendelea
kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe sambamba na Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Waziri Membe na Dr. Migiro wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya mkutano na waandishi wa habari.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati),
akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania baada ya kumaliza
muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na
mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na siasa kwa sasa. Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe
na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta
jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa
Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
Pichani Juu na Chini ni wakinamama
wakimwimbia Happy Birthday Dr. Asha Rose Migiro ikiwa ni maadhimisho ya
siku yake ya kuzaliwa aliporejea nyumbani leo.
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dr. Migiro (hayupo pichani)
Dr. Asha Rose Migiro akizungumza Jambo
na Dr. Alberic Kacou wakati wakitizama burudani ya ngoma iliyoandaliwa
maalum kwa ajili yake. Kushoto ni Waziri Membe.
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
"Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dr. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi
mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha
ametua nchini Salama.
--
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
(UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani
leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo
wa siasa.
Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk.
Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya
siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara
la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa
anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana
na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment