• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, July 4, 2012

    Breaking Newzzz.........MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST.AGREY MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI


    Samahani kwa picha hizi



    Hii ndiyo pikipiki inayodaiwa mwanachuo huyo kuiiba

    Hiki ni kitambulisho cha mwana chuo huyo



    Mwananchuo wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole jijini mbeya
     anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali 
    katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki zakusafirishia abiria
     maarufu kama bodaboda. 

    Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa
     huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati 25 mpaka 30 . 

    Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8
     za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea
     isanga jijini mbeya. 

    Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za
     kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya
     chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi 
    wa Ilomba jijini hapa

     
    Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa
     kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea
     nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la isanga akielekea barabara ya
     chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wanainchi wenye hasira kali nakuanza
     kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai

    No comments:

    3500K