Mwili wa Marehemu Mtoto mchanga ambaye hayafahamika mama yake amekutwa ametupwa karibu na Msikiti wa Soweto Mbeya Asubuhi hii.
Wakazi wa eneo hilo wakiwa wamefika kushuhudia Kichanga kilicho tupwa eneo la Soweto Mbeya asubuhi hii
Picha
ya juu na hii ya chini ndivyo zinavyo onekana baada ya mtoto huyo
kufumuliwa kutoka kwenye mfuko huo wa salfet unao onekana akiwa amesha
fariki, Hiyo nguo ni msamalia mwema ametoa
Polisi wamesha fika eneo la Tukio na kuchukua mwili wa mtoto huyo asiye na hatia
Polisi akiwa wanaonekana anaondoka na Mwili wa Marehemu eneo la tukio
Mbele ni Msikiti wa Poilisi ambao unaonekana na Huku Polisi akiendelea na safari
Baadhi ya mashuhuda wakitazama mtoto akiondolewa eneo hilo
Polisi Ndio wanaondoka eneo la tukio sasa
**************
Katika
hali ya kutatanisha wananchi wa Soweto jijini Mbeya wamekutana na
Kifurushi ambacho ndani yake kulikuwa na mtoto mchanga amewekwa na
kutupwa akiwa amefariki, ikiwa ni tukio la pili kutokea eneo hilo baada
ya tukio kama hilo kutokea wiki mbili zilizopita.
Hata
hivyo akiongea na baadhi ya wananchi ambao hawakupenda kutaja majina
yao wamedai kwamba kuna dispensary jirani hapo ambayo hawakutaka sema ni
hospital ipi ambapo wana wasi wasi kwamba hutoa Mimba mabinti na
kuwatupa eneo hilo.
Mbeya yetu tunafanya uchunguzi wa kina kama ni kweli maelezo ya wadau na tunafuatilia kama kweli Dispensary hiyo ipo.
No comments:
Post a Comment