M
|
cheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye
alitua mjini Moshi jana kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro
Marathon jana amekaa na watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa
na masista wa shirika la Precious Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa
kishindo katika Manispaa ya Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini
Marekni kwa kutumia usanii wake wa filamu.
Deidre Lorenz anashiriki katika
mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua vumbi tarehe 24
Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi. Mbio za Mt.
Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na
balozi wa zamani wa Tanzania
nchini Misri kuja Tanzania
kuanzisha mbio za marathon.
Deidre Lorenz anawakilisha
kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya
kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto yatima
cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto. Aidha,
aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na
zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.
Lorenz ameshiriki pia katika
mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza kuhusu nia
yake ya kuitembelea Tanzania
mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura nzuri
sana. Aidha
marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje katika mbio
zinazofuata.
Klabu ya Mt. Kilimanjaro
Marathon 1991 inakusudia kuwatumia watu maarufu kuja Tanzania ili waweze kuutangaza
utalii pamoja na mazingira ya kuwekeza. Klabu hii ina lengo la kuanzisha
marathon nyingine tena ambayo itajumuisha mbio na michezo mingine ya uwanjani.
Akielezea kuhusu mikakati ya
klabu yake kuendeleza mchezo wa riadha Ngowi ambaye pia ni Rais wa IBF/USBA
katika bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi alisema kuwa
wameweka mikakati mingi itakayoifanya mji wa Moshi kuwa kitovu cha utalii
katika mkoa wa Kilimanjaro.
Hizi mbio ni sehemu tu ya
mikakati ya kuendeleza michezo katika mkoa huu ambao miaka ya sabini ulikuwa
unaongoza kwa michezo katika nchi hii. Alisema kuwa wameandaa mikakati mingi na
kumalizia kuwa Tanzania
ni yetu sote kwa hiyo tuna jukumu la kuchangia katika maendeleo yake.
Deidre Lorenz atakimbia
mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili ijayo na ataondoka usiku wa jumapili
kurudi nyumbani kwake New York jiji
linajulikana kama “The Big Apple” na Financial
Capital of the World (Jiji la Fedha Duniani)
Imetumwa na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano
Mt. Kilimanjaro
Marathon
Technology House
35-38 Ghalla Road
Moshi - Tanzania
No comments:
Post a Comment