TEKNOLOJIA ya kutumia simu kufukuza
mbu nyakati za usiku imeingia nchini.Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM), Gerald Simbo aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba simu yake ina
uwezo wa kufukuza mbu usiku inapowekwa kwa kutumia mfumo wa 'Mosquito
repellant'.
Simbo alisema simu yake inayojulikana kwa jina la "Samsung Galaxy
Pocket ina uwezo wa kufukuza mbu kama itawekwa
kitandani wakati wa kulala. Amesema simu hiyo aliinunua kwenye kampuni SamSung Tanzania.
Meneja wa Samsung Tanzania,
Kishor Kumar alipoulizwa jana kuhusiana na kauli hiyo alikiri kuwa na aina hizo
za simu na kwamba sasa zinasambazwa nchini na kuuzwa kwa gharama ya Sh200,000.
Naye mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Enock Kweka amesema
anaitumia simu ya aina hiyo kufukuza mbu nyumbani kwake na kuhifadhi
nyaraka muhimu anazotumia katika masomo yake.Imeelezwa kwamba ina
mtandano wa kompyuta wa 250 MB kwa muda wa mwaka mmoja
Saturday, June 16, 2012
Home
Unlabelled
TANZANIA SOCIO-ECONOMIC NEWS: SIMU YA KUFUKUZA MBU YAINGIA
No comments:
Post a Comment