C
|
HAMA cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema), kimelaani kukamatwa na kushambuliwa kwa viongozi wa
madaktari ikiwamo Dk Ulimboka Steven ikieleza kuwa hatua hiyo haiwezi kuwa
suluhu bali itachochea zaidi mgogoro wa madaktari na Serikali.
Taarifa
iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika
inaeleza pia kwamba udhaifu wa Serikali kuharakisha kwenda mahakamani kabla ya
Bunge kupewa fursa ya kujadili madai ya madaktari na kuisimamia Serikali
umelifikisha taifa katika hali iliyopo sasa.
Mnyika amesema kuwa ameomba wabunge wapewe nakala ya Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu madai ya madaktari na hoja ya taarifa husika iwekwe katika orodha ya shughuli za Bunge katika mkutano wa Bunge unaoendelea ili ijadiliwe na kupitisha maazimio, kuwezesha hatua za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kuupatia ufumbuzi mgogoro huo na kuboresha sekta ya afya nchini.
Aidha
Mnyika amesema ikiwa wabunge wataelezwa ukweli na kupewa taarifa kamili wataweza
kuisimamia Serikali na kuwaeleza ukweli madaktari kipi kinawezekana na kipi
hakiwezekani. Mnyika amesema kuwa ameomba wabunge wapewe nakala ya Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu madai ya madaktari na hoja ya taarifa husika iwekwe katika orodha ya shughuli za Bunge katika mkutano wa Bunge unaoendelea ili ijadiliwe na kupitisha maazimio, kuwezesha hatua za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kuupatia ufumbuzi mgogoro huo na kuboresha sekta ya afya nchini.
Amesema kuwa ingawa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametoa maelezo bungeni kuwa Serikali itatoa kauli bungeni kuhusu mgomo huo, Bunge halitaruhusiwa kujadili kauli husika, hivyo kukoseshwa fursa ya kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi.
No comments:
Post a Comment