NI SINZA-MORI, DAR
Tukio hilo lililokuwa kama filamu ya kivita lilijiri nyumbani kwa mzazi huyo wa Wema, maeneo ya Sinza-Mori, Dar es Salaam Juni 20, mwaka huu, mchana kweupe wakati kukiwa na marudio ya kipindi alichotumia kumnadi mwanaye na kuwananga marafiki zake.Baada ya kugonga geti na kukaribishwa ndani na binti waliyemkuta, mapaparazi hao wawili walisimama kwenye mlango wa nyumba kusubiri binti huyo akamuite mama Wema ambaye wakati huo alisikika kupitia dirishani akimsimulia mtu kwenye simu yaliyojiri baada ya kubwatuka runingani siku moja iliyopita (jana yake).
“Eee! Nakwambiajee, nimewachamba ile mbaya kwenye televisheni na nimewaambia wasikanyage nyumbani kwangu,” alisikika mama Wema wakati binti aliyekwenda kumwita akisubiri amalize kuzungumza na simu amwambie kuna wageni wake (waandishi wawili).
‘MUVI’ LA KIVITA LAANZA
Sekunde kadhaa baada ya kukata simu, yule binti alisikika akimpasha habari kwamba kuna wageni wake, ndipo alipochungulia dirishani na kugundua kama aliokuwa akiwazungumzia muda mfupi ndiyo wameingia baada ya kuwaona wakiwa na vitendea kazi kama kamera, notebook, vinasa sauti na kalamu.
Kwa macho ya kawaida aligundua anaowaona mbele yake ni waandishi lakini kwa mwendo wa kubwatuka kwa sauti, alianza kwa kuuliza pasipo kutoa nafasi ya kupewa majibu.
“Ninyi ni waandishi, si ndiyo eeh. Nauliza ninyi ni waandishi? Nimesema sitaki kuona mwandishi anakuja nyumbani kwangu. “Eeeh… Hamnijui eeeh, hamjui mashetani yangu, eeeeeeeeh… nyie ni…(akaporomosha matusi mfulululizo). Ama kweli nyie vichwa ngumu! Pamoja na kuchimba mkwara mmekuja!” alisikika mama Wema.
BINTI AWATIMUA WAANDISHI
Mama Wema alipogundua kwamba waandishi wako ‘fulu’ na vifaa vya kazi, ilibidi ‘amualati’ binti huyo awapopoe kwa mawe na kisha kuwasakizia mbwa ambaye alionekana si wa ulinzi (ni yule Fiona wa Wema).
MAHOJIANO KUPITIA DIRISHANI
Wakati akiendelea ‘kuwaka’ na kusababisha mtaa mzima kurindima, waandishi waliendelea kufanya naye mahojiano kupitia dirishani wakitaka majibu ya maswali yao yaliyohusiana na utajiri wa ghafla wa Wema lakini majibu yakawa ni kelele za mayowe kutoka kwa mzazi huyo.
Timu ya waandishi ilipojiridhisha kwa picha za kumwaga, iliondoka na kumwacha mama Wema akiendelea kuporomosha matusi akiwa chumbani.
Imeandikwa na Richard Bukos, Erick Evarist na Issa Mnally.
No comments:
Post a Comment