• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Saturday, June 30, 2012

    Alpha Awaponda Wadhamini Wa Tusker Project Fame


    Wakati mashindano ya Tusker Project Fame yakiendelea jijini Nairobi, Kenya, mshindi wa msimu wa tatu wa mashindano hayo Alpha Rwirangira kutoka nchini Rwanda, jana ameandika barua ndefu kuwashutumu wadhamini wa mashindano ya vipaji vya kuimba East Africa Breweries Limited, EABL.
    Hivi ndivyo alivyoandika kupitia ukurasa wake wa Facebook.

    Naandika barua hii nikiwa na uchungu mkubwa moyoni.  Mashabiki wangu wapendwa, inauma sana. Kwanza naishukuru EABL kwa kunitambulisha kwenye midani ya muziki. Lakini niruhusuni tena niseme kukatishwa kwangu tamaa. EABL inaingiza hela nyingi sana kutokana na washiriki hawa lakini bado haitaki kuwaunga mkono na kuwajali baada ya show. Ningependa kuwapa mfano wa Victoria Kimani, kama angekuwa mkweli na kuwaambia yote aliyoyapitia baada ya kushinda TPF1, ni aibu sana, kama EABL ingekuwepo kwaajili yake ninaamini Kimani angekuwa mbali sana na kipaji chake.
    Mwangalie Ester, ni aibu jinsi watu wengi wasivyojua kuhusu yeye na bado hawamjui mwimbaji huyu mwenye kipaji, natamani angesimulia story yake kutokana na njia aliyoipitia baada ya TPF2, ni aibu kubwa.
    Sasa kuhusu mimi, ni story ile ile naomba radhi kwa kusema hilo, hata hivyo sina cha kupoteza lakini EABL hili ni kubwa mnahitaji kuwasaidia wasanii wenu, msiwaache wakirandaranda kama kondoo waliopotea.  Mnachofikiria ni kuhusu ninyi wenyewe, inauma sana.

    Nakumbuka niliandaa show nyumbani Rwanda ambako nilileta baadhi ya wahusika wa TPF akiwemo jaji Ian, na niliwaomba EABL wadhamini show yangu wakapuuzia baada ya kuwaonesha ni kiasi gani ninajituma angalau kuwa mbunifu na kufanya nao kazi.

    Ni aibu kwamba nilidhaminiwa na makampuni mengine na EABL haikuwepo licha ya kuwa niliwafuata kuwaomba udhamini kama makampuni yote haya mengine. Waliendelea kunipa ahadi mpaka dakika ya mwisho, ni aibu na inauma.

    Na sasa mwangalie kaka yangu Davis, mpaka sasa hivi anahangaika na record deal, EABL sijui kinachoendelea kwenye mkataba wake kwakuwa hakuna kilichofanyika hadi sasa na TPF 5 inaendelea, unadhani watu hawa wanawatendea haki wasanii?

    Ninashangaa kwanini wanaendelea na TPF5 kama watakuja kufanya sawa na walivyotufanyia sisi sote? Sio haki. Tafadhali watu msinielewe vibaya lakini watu huwapigia kura wasanii wawapendao na wanapenda kuwaona wakikua na wasipoona kile walichotarajia huwalaumu wasanii, tafadhali naomba mniruhusu kuwaonesha akina nani wanaopaswa kulaumiwa. Inauma sana. Nimeviweka vitu moyoni mwangu lakini umefika muda niviseme, kwakuwa sina cha kupoteza lakini walau wacha niongee na wadogo zangu ili wasije kukutana na tatizo lile lile. Tafadhali mashabiki wetu tunaomba maoni yenu kuhusu suala hili.

    No comments:

    3500K