Wamisri wameanza kupiga kura katika
duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo kati ya mgombea
anayefuata siasa zinazoegemea dini ya Kiislamu dhidi ya waziri mkuu
wa zamani wa utawala wa taifa hilo huku kukiwa na hali ya wasiwasi na
wakati hali kisiasa baada ya mageuzi haieleweki.
Ahmed
Shafiq, waziri mkuu wa mwisho wa rais alieondolewa madarakani Hosni Mubarak
anapambana na mgombea wa chama cha Udugu wa Kiislam, Mohammed Mursi katika
zoezi la kupiga kura litakalodumu kwa siku mbili ambapo kiasi ya raia milioni
50 wamejiandikisha kushiriki zoezi hilo.
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema asubuhi ambapo kiasi ya askari
150,000 wametawanywa kwa nia ya kudhibiti hali ya usalama
kwenye uchaguzi huo wenye mgawanyiko mkubwa. Kinyang'anyiro hicho kimeleta
mtengano na hasa kwa wale wenye hofu ya kurejea madarakani kwa uongozi wa
zamani kupitia Shafiq na wale wanaotaka kutenga siasa na dini na shaka
kwamba chama cha Udugu wa Kiislamu kitavuruga uhuru wa watu. Katika
duru ya kwanza ya uchaguzi huo Mursi alipata asilimia 24.7 ambapo Shafiq ambae
pia alikuwa kamanda wa jeshi la anga alipata asilimia 23.6 ya
kura.
Saturday, June 16, 2012
Home
Unlabelled
AFRICA NEWS: WAMISRI WANAPIGA KURA LEO
No comments:
Post a Comment