‘ACTION…camera roll’ ndiyo maneno ambayo wasanii huyatumia mara kwa mara wanapokuwa lokesheni, eneo ambalo wanalitumia kurekodi kipande fulani cha sinema zao. Huwa wanayatamka maneno hayo ili waweze kuuvaa uhusika wa kifi lamu. Yaani kama anatakiwa kuonekana analia, msanii ajitoe ufahamu kwa muda ili aonekane analia mbele ya kamera. Mathalani, anaweza kuvaa uhusika wa tabia za mlinzi wakati yeye si mlinzi. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba anachokifanya pindi anapoambiwa maneno hayo huwa si uhalisia. Anakuwa anaigiza. Anavaa uhusika wa jambo fulani baadaye anarudi kwenye hali yake ya KAWAIDA
No comments:
Post a Comment