Pages - Menu

Thursday, March 24, 2016

STARS YAICHAPA CHAD 1 DJAMENA

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imeibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya wenyeji Chad katika mchezo uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Omnisport Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena. Kikosi cha Stars kilicheza vizuri kwa maelewano kwa lengo la kusaka bao la mapema, safu ya ushambuliaji ilikuwa mwiba kwa walinzi wa Chad katika dakika 30 za kipindi cha kwanza na kukosa nafasi zaidi ya nne za wazi kupitia kwa Ulimwengu, Farid, Samatta na Kazimoto

No comments:

Post a Comment