Pages - Menu

Thursday, March 24, 2016

Linah Sanga Natamani Kuwa na Mahusiano na Wizkid

Akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana (EATV) Linah Sanga alisema kuwa toka kipindi cha nyuma alikuwa anatamani kuwa na msanii huyo kama mpenzi wake, ingawa anadai mpaka sasa ndoto yake hiyo haijaweza kukamilika mpaka dakika hii. "Unajua nilikuwa namu admire Wizkid toka muda mrefu, na ndiyo mwanaume ambaye hata ukiniuliza ni msanii gani wa kiume katika bara la Afrika ambaye ungependa kuwa naye au ambaye nampenda nitakwambia ni Wizkid, siwezi kukataa ila ndiyo hivyo tena maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli" alisema Linah Sanga

No comments:

Post a Comment