Diana Exavery ‘Malaika’.
STAA wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza
amefungukia ishu yake ya kuolewa ambapo amesema kwa sasa hayupo tayari na
kwamba bado yupoyupo kwanza.
Malaika mwenye shepu f’lan ‘amaizing’, aliitonya kona hii kuwa japokuwa
anaishi na mchumba wake lakini hilo halimfanyi kufikiria kuolewa akiamini
muda wa kuitwa mke rasmi bado.
“Mimi si wa kuolewa sasa bwana! Hapana siwezi kusema nipo tayari, bado
niponipo kwanza. Siku ikifika nitawaambia lakini si sasa, nahisi bado
muda…si unajua mambo mazuri hayataki haraka?” alisema Malaika
No comments:
Post a Comment