Kila la heri mwana; Mrisho Ngassa alikutana na Diamond Plutinumz jana jioni
kwenye Ndege wakati timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars
ikisafiri kutoka Mombasa kwenda Nairobi, tayari kwa mchezo wa Nusu Fainali
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya
wenyeji, Kenya Jumanne Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Stars ilicheza na Uganda juzi, The Cranes Uwanja wa County ya Mombasa,
zamani Manispaa na kuitoa kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya
dakika 90, wakati Diamond alifanya onyesho usiku wa siku hiyo ufukwe wa Big
Tree Resort,
No comments:
Post a Comment