• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Monday, November 4, 2013

    Janjaro kuyagusa mawimbi ya radio na kitu kipya mwezi huu, asema fans watamsaidia kuchagua jina

    Mambo yametulia kama zamani na kazi inaendelea kwa upande wa Janjaro, ikiwa ni siku chache baada ya Ostaz Juma kutangaza kumuondoa  ‘Watanashati’ na kumrudisha tena siku iliyofuata.
    Baada ya kuyatuliza mawimbi ya kutoelewana na Boss wake, sasa Janjaro atayagusa mawimbi ya radio na kitu kipya mwezi huu.
    Janjaro amefunguka jana (November 3) kupitia ‘The Playlist’ ya 100.5 Times fm wakati akiongea na Omary Tambwe aka Lil Ommy huku akizichagua ngoma tano anazozikubali.
    Mkali huyo toka Arusha amesema anatarajia kuachia ngoma mpya November 23, itakayopikwa na Producer Pancho Latino ndani ya studio za B Hitz, na kwamba atawapa fans wake nafasi ya kuchagua jina la ngoma hiyo.
    “Sasa hivi watu watarajie ngoma mpya, wataibariki jina mashabiki, ni ngoma ambayo nafanya kwa Pancho Latin.  Tumeshatengeneza mdundo kwa hiyo ni mimi tu kwenda kuingiza vocal, lakini kwenye tarehe 23 mwezi huu hivi itatoka na Times fm watakuwa wanaitambulisha, tuombe Mungu.” Amesema Janjaro.
    The Playlist ya 100.5 Times fm inakuwa hewani kila jumapili, saa kumi kamili hadi saa kumi na moja jioni.
    Unaweza kusikiliza pia kupitia tovuti hii kwa kubofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen Live’.

    No comments:

    3500K