NA JAIZMELALEO
Watu wawili wamefariki
dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo tukio la mtu
mmoja kupigwa risasi ubavuni na kufariki dunia papo hapo na watu wanao sadikiwa
ni majambazi wilayani Hai.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamanda wapolisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, amesema kuwa tukio hilo limetokea
hivi karibuni katika eneo la Machame
Wari wilayani hai.
Boaz amesema kuwa awali kundi hilo la
majambazi wapatao wanne walivamia kiosiki cha mfanyabiashara Emanuel Poul
ambapo walifanikiwa kupora fedha zote za mauzo na kumpiga risasi Mustafa
Ramadhani (45) na kufariki dunia papo hapo.
Aidha kamanda Boaz amesema tukio hilo
lilikuja siku chache baada ya kundi hilo la majambazi kumvamia mfanyabiashara
Matei Tumbo ambapo walifanikiwa kumpora bunduki yake aina ya Short
Gun na gari lenye nambari T264 ABY aina ya Toyota korola.
Amesema kuwa majambazi hao walipora
bunduki hiyo na kukimbia na gari hilo kabla ya kwenda kwenye uhalifu na
kumuua mfanyabiashara huyo .
Boaz alisema kuwa katika tukio hilo jeshi
la polisi limefanikiwa kuwakamata watu wawili wanao sadikiwa kuhusika na tuki
hilo ambapo waliwakuta wakiwa na risasi tatu za bunduki aina ya short Gun. Na
kwamba uchunguzi unaendelea ili kuwabaini watu wengine.
Katika tukio jingine kamanda boazi amesema
kuwa januari 20 mwaka huu wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kuna mtu moja aliye
julikana kwa jina moja la priscus alifariki dunia baada ya nyumba yake kuwaka
moto.
Amesema kuwa mtu huyo alifariki dunia
baada ya chumba alichokuwa amelala kuteketea kwa moto na kwamba chanzo cha moto
huo ni mshumaa alio kuwa amewasha kuangukia godoro na kuwaka moto.
No comments:
Post a Comment