Pages - Menu

Monday, January 21, 2013

OBAMA AAPISHWA

CHANZO::JAIZMELALEO

Rais wa Marekani Barack Obama amekula kiapo kwa ajili ya muhula wake wa pili jana, katika hafla ambayo ilihudhuriwa na wanafamilia na waandishi wa habari tu. 
 
Obama anaanza muhula wa pili akikabiliwa na matatizo kadhaa nyumbani na nje, yakiwemo mgawanyiko mkubwa mjini Washington kuhusu masuala mbalimbali, mpango wa Iran wa nyuklia, na wapiganaji wa Kiislamu katika kanda ya Afrika ya kaskazini. Mapema jana, makamu wa raia Joe Biden aliapishwa katika makaazi yake rasmi. Sherehe kubwa inatarajiwa kufanyika leo katika jengo la Capitol mjini Washington. Hotuba ya Obama inatarajiwa kujikita katika haja ya kufanya tahfif za kisiasa na warepublican pale inapowezekana.

No comments:

Post a Comment