Huyu ndiyo Diana Ibrahim Kisura wa Tanzania 2009 aliyeshinda katika
shindano la Kisura lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwene Hoteli ya
Movenpick jijini Dar es salaam
Mama Tunu Pinda katikati aliyeshika maua akiwa katika picha ya pamoja
na Kisura wa Tanzania 2009 Diana Ibrahim wa tatu kutoka kulia mara baada
ya kushinda kwenye shindano hilo lililofanyika jana kwenye Hoteli ya
Movenpick jijini Dar es salaam, wengine ni Jaji mark Bomani mwenyekiti
wa kampuni ya bia Serengeti wa kwanza kushoto na anayefuata ni mama
Janneth Massaburi Mbunge Viti Maalum Mkoa Dsm, kulia ni Juddy mwandaaji
wa Kisura na Teddy Mapunda mwenye kilemba Meneja uhusiano wa kampuni ya
bia Serengeti
Mgeni Rasmi mama Tunu Pinda akisoma hotuba yake katika shindano la
Kisura wa Tanzania lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa
kuamkia leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya
bia ya Serengeti Jaji Marck Bomani.
Kisura wa Tanzania 2009 Diana Ibrahim katikati akiwa na washindi
wenzanke Jaquiline Benson aliyeshika nafasi ya pili na Mwajabu Juma
kushoto aliyeshika nafasi ya tatu mara baada ya kwatangaza washindi
katika shindano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa
kuamkia leo.
Hawa ndiyo walioingia tano bora ya kisura wa Tanzania hapa wakipozi kwa picha.
Mavazi haya alibuni mbunifu Zamda George hayupo pichani, kila mrembo alivaa nguo iliyobuniwa kwa staili tofauti.
Visura wakipita jukwaani katika mavazi ya ubunifu kama unavyowaona katika picha.
Baby Madaha akionyesha umahiri wake katika kumiliki jukwaa kwenye shindano la Kisura wa Tanzania usiku wa kuamkia leo.
Wazee wa Goba Kalunde Band iliburudisha vyakutosha katika shindano hilo.
Mambo ya kikundi cha ngoma na sarakasi cha Splendid.
Hebu cheki pozi la Emma Mbaga kushoto na Grace Kilembe meneja mradi wa Kisura Tanzania.
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya simu za mkononi Zain Kevin Twisa kushoto na rafiki yake Amos Lwiza.
Mdau Bazo Komu wa TBC kushoto na Mtu mzima Wakuvanga wa Orijino Komedi.
Wadau wa Kisura wa Tanzania kutoka kulia ni Khadija Khalili Tazania
Daima, Ally Rehmtullah mbunifu wa mavazi , Teddy Mapunda na Nandi
Mwiyombela kutoka Serengeti.
Giva kushoto na Jamira visura wa mwaka jana 2008 nao walikuwepo.
Wadau Grace Kilembe kulia na rafiki yake nyuma kushoto ni mdau Willy Edward wa gazeti la Jambo leo na rafiki yake.
No comments:
Post a Comment