na suleman magoma blog
Zile death hoaxes zilizokuwa zikiwakumbuka wasanii wa Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwa wasanii wa Tanzania ambapo kumeanza kuzuka mchezo wa watu kuwazushia vifo wasanii wa Bongo.
Baada ya Profesa Jay kuzushiwa kifo wiki hii, Rama Dee naye amesema kuna watu wamezusha kuwa amefariki.Kupitia Facebook, Rama Dee ambaye kwa sasa yupo nchini Australia amelaani kitendo hicho na kuwataka ‘haters’ wasubiri mwenyezi Mungu aamue mwenyewe.
“Huu mchezo wa kuzushia watu wamekufa sio poa kabisa…inaonyesha ni jinsi gani akili yako ilivyo na matope ya ushamba na uchafu wa ulimbukeni….juzi mchizi wangu ametumiwa msg kuwa mimi nimedanja sio inssue subirini siku ikifika nikidanja mtapata habari ya kuandika kwenye page zenu Au blogs ila kwasasa punguzeni mizuka ya kise**e ni hayo tu asante,” ameandika mkali huyo wa R&B nchini.