na jaizmelaleo
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless
Lema, ameifunga Shule ya Sekondari Korona iliyopo Kata ya Engutoto jijini
hapa, ambayo ilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, mwaka
2011.
Lema
alifikia uamuzi huo katika kikao cha pamoja cha mashauriano shuleni hapo na
Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Eusebi Maeda, kilichohudhuriwa pia na Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji ambaye ni Ofisa Utumishi, Eliphas Mollel na Ofisa Elimu
Sekondari, Violet Muwowoza.
Alisema
kuwa aliifunga shule hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi
yaliyosababisha wanafunzi kushindwa kusoma tangu ifunguliwe Januari 14, mwaka
huu.
Matatizo
hayo ni pamoja na umbali unaosababisha wanafunzi na walimu kutembea kilometa
6.5 hadi kufika shuleni hapo, hivyo kuwa na muda mfupi wa masomo.
Shule
hiyo pia haina huduma ya maji safi baada ya bomba lililokuwepo kukatwa na
mamlaka ya maji kutokana na deni la sh 340,000. Pia, pamoja na walimu watano
waliopo, mkuu wa shule na msaidizi wake hawaonekani.
Kati
ya wanafunzi 1,200 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu wa shule hiyo ni
wanafunzi 118 pekee ndio wanaohudhuria masomo.
No comments:
Post a Comment