Vladimir Franz ni mmoja kati ya wagombea tisa wa kiti cha Urais Jamhuri ya
Czech ambaye asilimia 90 ya mwili wake umechorwa 'tattoo'.
Pamoja na hilo kura za maoni zimempa 11.4% ya kura zote ambapo amekua ni
mgombea wa tatu kati ya wagombea hao 9. Franz mwenye umri wa miaka 53 ana
shahada ya sheria, ni profesa wa fani ya maigizo pia ni mchoraji.
Franz alisema kuwa 'tattoo' ni jambo lake binafsi, halina uhusiano na
kugombea kiti cha Urais. Pia ushindani wa kiti cha Urais siyo shindano la
urembo.
No comments:
Post a Comment