Krismasi (pia Noeli)
ni sikukuu
ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo
zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba
katika Ukristo
wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Historia ya Krismasi
Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa
sababu utamaduni
wa Wayahudi
wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Lakini
baadaye Ukristo
ulienea katika Dola la Roma na kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida
ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia
sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya Sikukuu ya Krismasi.
Tangu
mwanzo wa karne
ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya
kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari
za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana
kutoka Misri mnamo
mwaka 200. Mwandishi
Mkristo Klemens wa Alexandria (kitabu cha
Stromateis I, xxi) alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri
waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia
kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja
na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Labda
kadirio la tarehe ya Desemba 25 pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200
(kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus)
tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi
ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya kuzaliwa kwake. Kwa kuongeza
miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
Inaonekana
tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25
Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Wataalamu
mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe
hiyo kwa nia ya kuchukua nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol
invictus". Lakini pengine mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari
walianzisha sikukuu hiyo halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili
kushindana na Ukristo
uliokuwa bado chini ya dhuluma.
Aliyeingiza
sikukuu ya Kuzaliwa Jua (Mitra) huko Roma ni Eliogabalus (kaisari kuanzia 218 hadi 222). Baadaye Aurelianus akaithibitisha rasmi
mwaka 273, hatimate
ikahamishiwa tarehe 25 Desemba. Wakati wa Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa
ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba. (Taz. maandishi yaliyotajwa na Allan S.
Hoey katika ukurasa 480 (rejeo 128) wa Official Policy towards Oriental Cults
in the Roman Army, Transactions and Proceedings of the American Philological
Association (70) 1939, pp 456-481).
Wakristo
wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki, Waprotestanti,
sehemu ya Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe
nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda.
Habari za Krismasi katika Biblia
Habari
za Krismasi kama sherehe hazipatikani katika Biblia kwa sababu
zilizotajwa hapa juu.
Lakini
hasa vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo
na Luka.
Katika Injili ya Mathayo
Mathayo
anasimulia habari hizo katika mlango wa kwanza kuanzia aya 18 na katika mlango
wa pili.
Bikira
Maria alipata mimba wakati alipokuwa mchumba wa Yosefu. Yosefu alitaka
kumwacha lakini aliambiwa na malaika aanze kuishi naye na kumkubali mtoto kama wake kwa
kumpa jina "Yesu".
Mamajusi kutoka
mashariki
waliwatembelea na kuwaletea zawadi kwa sababu waliona nyota ya pekee
iliyokuwa kwao alama ya kuzaliwa kwa mfalme mpya katika Uyahudi
ikawaongoza hadi Yerusalemu. Lakini walipompitia mfalme Herode Mkuu,
huyo alikasirika akimwogopa mfalme mpya. Hata hivyo aliwaelekeza Bethehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.
Yosefu
alipata tena ujumbe kutoka kwa malaika akaondoka na mtoto na Maria kukimbilia Misri kabla ya
askari wa Herode hawajaweza kumuua Yesu.
Baada
ya kifo cha Herode
walirudi kutoka Misri lakini hawakuenda tena Bethlehemu bali kuhamia Nazareti katika
mkoa wa Galilaya.
Katika Injili ya Luka
Katika
taarifa ya Luka (mlango wa 1 na 2) Maria
alipokea huko Nazareti ujumbe wa malaika
mkuu Gabrieli kwamba atapata mimba na mtoto
wa pekee.
Yosefu
na Maria walikwenda Bethlehemu kwa sababu ya sensa iliyowataka
kwenda katika mji alikotokea Yosefu. Hapo Yesu alizaliwa katika hori la kulishia wanyama; wachungaji
mabondeni walitangaziwa na malaika habari hiyo wakaja kumwona mtoto.
Baada
ya kuzaliwa wazazi walimpeleka Yesu Yerusalemu katika hekalu kufuatana na
sheria ya Agano la Kale (Kitabu
cha Kutoka 13,2; 13,15) halafu wakarudi kwao Nazareti.
Habari za Krismasi katika Korani
Sura
ya tatu (Al Imran, 42-47) ina habari za tangazo la malaika kwa Bikira Mariamu
zinazofanana na Luka 1.
Sura
ya 19 (Mariamu, 16-34) inarudia tangazo la malaika kwa Mariamu na inasimulia
kuzaliwa kwake Yesu chini ya mti wa mtende, halafu majadiliano kati ya Mariamu na ndugu zake.
Mtoto mchanga Yesu akaanza kusema wakati wa kuzaliwa akimtetea mama yake dhidi
ya ndugu zake.
Krismasi katika maisha ya binadamu
Watu
wote ni wakosefu na kujenga mazingira maovu hata wanayakinai na kutamani wamuone mtu
tofauti, yaani mwema na mtakatifu. Pengine wanadhani fulani ni mwema kabisa, kumbe
siyo.
Haja hiyo inaturudia sisi: kwa nini nisiwe
mimi mtu wa namna hiyo? Kwa nini nisianze na moja kama kwa kuzaliwa upya kabla sijawadai
wengine? Zaidi tena, haja kuu ya binadamu ni kumuona Mungu mwenyewe:
lakini wapi, lini, namna gani?
Krismasi katika liturujia
Kama
kawaida, imani na liturujia ya
Kikristo zinaitikia haja za binadamu. Kipindi
cha Noeli kinatimiza haja tulizozitaja, kwa kuwa anazaliwa mtu mpya kabisa
ambaye anatuvutia kwa wema wake na ambaye tukimuona tumemuona Mungu, tena
tukimpokea tunazaliwa upya kama wana wa Mungu.
“Leo
amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”. Tunapoadhimisha Noeli tangazo
hilo la malaika kwa wachungaji linatufikia sisi. Si kujidanganya, kana kwamba
Yesu angezaliwa leo, wala hatukumbuki tu tukio la zamani, bali fumbo la
kuzaliwa Bwana linatufikia leo katika liturujia na kutuletea neema zake. Hivyo
tunaweza tukazaliwa upya kwa kushiriki kuzaliwa kwa kichwa chetu.
Liturujia
inashangilia hivi, “Lo! Mabadilishano ya ajabu! Mwana wa Mungu anakuwa mtu
kusudi mtu awe mwana wa Mungu!”. Tena si binadamu tu, bali viumbe vyote
vinapata heshima mpya kwa Neno wa milele kujifanya kiumbe.
IMEANDALIWA NA JOHNSON JABIR KWA MSAADA WA MTANDAO
No comments:
Post a Comment