Kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Decemba 7 2012 R’n'B star wa bongo Makamua aliongea ukweli kwamba mwaka huu uongo mkubwa alioufanya ni kudanganya kwamba single yake ya ‘bado kujuana’ amemshirikisha Super star Akon.
Alisema huo uongo wakati bado video haijatoka ila ukweli ni kwamba hajamshirikisha Akon bali ni Mtanzania anaitwa Eddo ambae kidogo ana sauti kama ya Akon, hii video hapa chini ndio ya hiyo single na huyo Eddo yuko ndani pia, itazame alafu uniambie umeipokeaje mtu wangu.
No comments:
Post a Comment