• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, November 13, 2012

    Sakata la Waliogandana Temeke Chanzo ni Mchungaji


    SAKATA la watu wanaodaiwa ni wanandoa wasaliti kugandana, Temeke, Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa, Mchungaji John Mzule wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala, Dar naye alichangia kuenea kwa uvumi ule, hivyo polisi wanamfuatilia. Mchungaji Mzule ameingia matatani baada ya kudaiwa kuwa, siku ya tukio aliushawishi umma uamini kwamba kuna watu waligandana wakifanya zinaa kwa vile alithibitisha kuwa, aliwaona wazinzi hao wakishushwa kutoka kwenye gari aina ya Canter hospitalini Temeke. Mchungaji huyo alikuwa akithibitisha hayo katika eneo la hospitali hiyo pale alipohojiwa na mapaparazi hali iliyowafanya watu waliokuwa wakimsikiliza kuamini hivyo na wao wakawapigia simu wenzao kutoka pande mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ambao walifika kwa lengo la kushuhudia. Katika eneo la tukio, mwandishi wetu alimkuta Mchungaji Mzule akimlaumu mtu aliyesababisha ‘wazinzi’ hao kugandana kwamba, alifanya kosa kubwa sana na anastahili adhabu ya pekee atakapobainika. TUNAMNUKUU: “Kitendo hiki ni cha kinyama sana na aliyesababisha hapaswi kuvumiliwa kwa sababu ni udhalilishaji wa kijinsia.” Uwazi lililokuwepo hospitalini hapo siku ya tukio, lilishuhudia wananchi wakiwa wamefurika wakitaka kushuhudia watu hao waliogandana licha ya kuambiwa na uongozi wa hospitali kwamba hakukuwa na tukio hilo. Baadhi ya maafande wa Jeshi la Polisi waliozungumza na waandishi wetu Novemba 9, 2012 walisema mtu aliyevumisha habari hiyo kama akijulikana atachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kuuadaa umma. “Ni kwamba kama tutampata mchungaji huyo au mtu mwingine anayechangia kueneza uvumi huu ni lazima tutamhoji atueleze kwa nini amezusha,” alisema afisa mmoja wa cheo cha juu wa polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Angelbert Kiondo alipopigiwa simu siku ya Jumapili ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo, iliita bila kupokelewa.

    No comments:

    3500K