JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock
Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye
umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma,
Wilaya ya Momba, mkoani hapa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba
mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa
kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi
ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya
kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo
unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho
chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo
alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia
kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa
dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
Wakati huohuo, katika kijiji cha Malangali
Barabara ya Mbeya-Iringa, Wilaya ya Mbarali gari aina ya Nissan Patrol
lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa mwili wa marehemu bado haujafamika na
mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi
za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.
No comments:
Post a Comment