Msanii wa Taarabu Mariam Khamisi aliyekuwa akiimba TOT mwenye
Tisheti nyekundu pichani ndiye aliyefariki dunia wakati akijifungua
katika hospitali ya Muhimbili.
Msanii wa muziki wa taarab
nchini Tanzania wa kundi la Tanzania One Threter TOT, Mariam Khamis
maarufu kama paka mapepe amefariki dunuia usiku wa jana kuamkia leo
katikam hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa baba mzazi
wa marehemu Khamis Muhidini Shomary Maria Khamisi alifariki kwa kifo
cha uzazi mara baada ya kujifungua hospitalini hapo.
Mariam enzi za uhai wake
aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarab
likiwamo East Africa Meldy ambapo alirikodi kibao kilichomfanya
kulikana kilichokwenda kwa jina PAKA MAPEPE, makundi mengine ni
Zanzibar Stars ambapo alidumu kwa muda mrefu huku akitamba na vibao
kama Narindima naye, Raha ya Mapenzi na nyinginezo.
Alipokuwa 5stars mariam
alitamba na nyimbo kama Ndo Basi tena, Uzushi hauniitii Doa na
baadaye alimua kuhama katika kundi hilo na kwenda TOT ambapo
alirikodi kibao kilichikwenda kwa jina la SIDHULIKI NA LAWAMA, na
alidumu hapo mpaka umauti ulipomfika.
Mipango ya mazishi
inaendelea kufanyika ambapo anatarajiwa kuzikwa kesho Magomeni Kota
jijini Dar es Salaam. Pole kwa marafiki,ndugu na wapenzi wa muziki wa Taarab nchini
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMENI
No comments:
Post a Comment