www.filexmmari1994.blogspot.com |
Add caption |
Staa kutoka ’game’ ya muziki wa kizazi kipya Bongo, Herry Samir ‘Mr
Blu’ amesema nguvu ya zaidi ya 10 aliyoiweka kwenye fani hiyo sasa
imemfanya kumiliki kiasi kikubwa cha ‘ngawira’ za kibongo (Shilingi).
Katika Interview ya dakika 45 aliyoifanya na teentz.com, juzi kati,
Blu ambaye sasa yuko kwenye kilele cha Bongo Fleva akisumbua na ngoma
yake mpya inayobeba jina la ‘Nipende kama nilivyo’ alifunguka kuwa si
mara moja mtu anaweza kuzungumza juu ya kile kinachomhusu kama
anachokifanya yeye lakini ameamua kufanya hivyo kwa lengo la
kuwaonyesha watu kuwa kile wanachokifanya wasanii ni kazi ama bishara
kama zilivyo zingine.“Kwanza, nashukuru kwa kuwa umenifuata na kuniuliza mambo kama hayo, ukweli ni kuwa nafahamu ni ngumu kwa mtu kuzungumza juu ya vitu kama hivyo lakini kwa kuwa tunachokifanya wasanii ni kazi kama zilivyo zingine sina tatizo nitakujibu kila kitu katika ukweli na kwa ufupi sana” alisema Blu.
Akiendelea Blu ambaye pia mashabiki wake hupenda kumuita ‘Babylon Baysser’ alisema kufanikiwa kwa wimbo wake wa kwanza ‘Niite Mr Blu’ ndiyo ulikuwa mwanzo wa mafanikio licha ya matatizo kadhaa aliyokutana nayo mara baada ya kupata umaarufu.
“Kulikuwana matatizo mengi sana baada ya kufanikiwa kwa ngoma hiyo, lakini nashukuru Mungu kuwa ndani ya muda wote huo nimefanikiwa kujenga nyumba yangu,kununua gari, na pia akaunti yangu kwa sasa iko poa sana”,
“eee ndiyo natarajia kuoa, na kwa kuwa tayari nina mtoto haina shaka kuwa mama mtoto wangu ndiye nitakayempa heshima hiyo” kwa hiyo hicho ndiyo ninachoweza kusema kuwa huo ndiyo utajiri wangu ndani ya miaka zaidi ya 10 kwenye gemu kwa kuwa nimetumia nguvu zangu kupata vitu hivyo vyote na siku zote Mungu amekuwa akinisimamia” alisema Blu.
No comments:
Post a Comment