Msanii wa kundi la N2N Lord Eyes
Msanii wa kundi la Nako2Nako Lord Eyes ambaye hivi karibuni anatuhumiwa
kuhusika na wizi wa vifaa ya kwenye magari atazungumza na waandishi wa
habari kuhusu sakata zima hilo.Kwa mujibu wa msemaji wa Kundi la WEUSI
Nikki Wa Pili ambalo pia N2N ni member,alisema kuwa msanii huyo atatoa
maelezo ya kilichotokea na kujibu maswali yote siku ya Jumamosi saa 5 na
nusu maeneo ya Sinza BaraBara ya Sam Nujoma kwenye Hotel inayojulikana
kama Wistas.
Wasanii wa Kundi hilo la WEUSI G Warawara,Bonta,Joh Makini,Bonta na Lord Eyes kwa mbele
No comments:
Post a Comment