hemed by filex mmari |
UKWELI wa mambo juu ya msanii anayependa kulipuka pamba Hemed Suleiman
’Hemedi’ almaarufu kama PHD au Alejandro, umevuja kwani inadaiwa kuwa
nguo zote anazoonekana anavaa huwa anachukua kwa mkopo na hulipa baada
ya muda fulani lakini sasa kiasi cha fedha anachodaiwa ni kikubwa na
hana uwezo wa kulipa kwa sasa kwani ni zaidi milioni 1.
Duka moja la nguo maarufu sana lilipo maeneo ya Kinondoni, ndilo lililotoa ishu hiyo baada kuona jamaa huyo anazingua kulipa na walikuwa wakimpa kila nguo anayohitaji kwani walimuamini kwa kuwa nguo nyingi alikuwa akinunua hapo kwao.
Muuzaji wa pamba hizo katika duka hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe na duka pia, alisema kuwa awali jamaa alikuwa akilipa kama kawaida lakini ilifika kipindi alikuwa anachukuwa kila baada ya wiki na hadi hivi sasa anadaiwa si chini ya milioni 1.
“Hemedi tunamuamini lakini sasa hali hii inafikia kuwa vita kwa sababu kiasi cha fedha tunachomdai ni kikubwa kwa sababu watu wanafanya kazi wanahitaji kulipwa mshahara, tunafikilia kuchukua maamuzi ili aweze kutulipa kwa haraka. Jamaa sikuhizi haji hapa na wala sijamuona kupita sasa sijui anakimbia madeni au vipi,” aliongeza
Hata hivyo Hemedi alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo kama ina ukweli wowote hakuweza kupatikana na taratibu zinaendelea za kumtafuta ili aweke wazi juu ya habari hizo.
Credits to Dartalk

No comments:
Post a Comment