• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, November 7, 2012

    Dallas wa Wolper Achoka-Ageuka Omba Omba






    MFANYABIASHARA ‘mjanjamjanja’, Abdallah Mtoro ‘Dallas’, amefilisika na amechoka vibaya kiasi cha kuanza kuombaomba bia.
    Mwanasiasa aliyeshinda ujumbe wa Nec (CCM) hivi karibuni, William Malecela ‘Le Mutuz’, aliandika wiki iliyopita kwenye ukurasa wake, mtandao wa kijamii Facebook: “Ok I have this friend, Super Dallas anatokea sana kwenye magazeti. I feel sorry for him aliwahi kuwa na utajiri wa ajabu alikuwa akihonga Mabebs wa mjini mpaka USD 10000 (karibu shilingi milioni 16).



    “Then akawa mchumba wa Wolper! Poor guy now amechacha watu wote hawamtaki wanamkimbia waziwazi na kumcheka, I feel so bad for him siwezi kumkimbia I know him, so I accommodate him like I know nothing people get upset with me that kwa nini ninam support na kumpa vinywaji?”
    William ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, John Samuel Malecela, alichanganya Kiswahili na Kiingereza lakini alichomaanisha ni kuwa Dallas amefilisika kiasi ambacho yeye ndiye amekuwa akimlinda kwa kumnunulia vinywaji.
    Jitihada za kumpata Dallas azungumzie madai hayo ya William hazikufanikiwa lakini baada ya mwanasiasa huyo kuandika hivyo, watu wengi walinakili ujumbe huo na kuusambaza kwenye mitandao mbalimbali.


    Bloga mmoja wa kike, aliweka kwenye blogu yake huku akisindikiza kwa kichwa cha habari: “Maskini Dallas wa Wolper kutoka kwenye utajiri wa madola mpaka zero ground.” Akimaanisha kwamba mfanyabiashara huyo alikuwa tajiri akimiliki noti za dola mpaka kufilisika hadi sifuri.
    Wolper alipoulizwa kuhusu hali ya Dallas kama anaweza kumsaidia, alijibu: “Nisingependa kumzungumzia huyo mtu.”

    No comments:

    3500K