Mnazaleti alizungumza na DarTalk kuhusu jina la staa wa bongo movie ambaye anamzungumzia ndani ya ngoma hiyo, ndipo alipofunguka kuwa hawezi kumtaja mtu yeyote kwani ameshakula kiapo tangu alipokuwa anauandika wimbo huo.
Alidai kuwa watu wengi watu wana majibu yao lakini kwa upande wake hawezi kuzungumza chochote kwani anaamini hataki kumdhalilisha staa huyo kwa tabia zake za kumsubua kwenye simu wakati awali alikuwa anamuona kama kuku mchafu.
“Watu wengi wamekuwa na majibu yao kuwa ninayemuimba ni kati mtu fulani au fulani lakini kwa upande wangu ni nimekula kiapo cha kutomtaja niliyemzungumzia hivyo nawaomba mashabiki wangu wajue kwamba hata kwa mtutu siwezi kumtaja jina atabaki kuwa siri yangu” alisema
No comments:
Post a Comment