Ni wiki mbili zimepita lakini
hii taarifa bado inaongoza kwenye headlines za Nigeria, ni kuhusu
wanachuo wanne ambao walipigwa, waliteswa, walitembezwa uchi barabarani
na baadae kuchomwa moto hadharani wakidaiwa kuwa ni wezi.
Imefahamika ni watuhumiwa 13 akiwemo chief wa hicho kijiji cha Aluu ambae alihusika pia kuwachoma moto hao wanachuo.
Watuhumiwa hao wamesema kulikua
na askari polisi mmoja ambae aliwaaambia wawachome moto hao wanachuo
wakati huohuo kulikua na askari mwingine aliesema wasichomwe moto.
Chanzo cha kuchomwa moto
kilitokana na mmoja kati yao kuwaomba wenzake kumsindikiza kwa jamaa
mmoja aliekua akimdai hapohapo kijijini lakini kibao kikawageukia baada
ya jirani wa mdaiwa kuanza kupiga kelele kwamba wamevamiwa na wezi,
vivyo hivyo kwa mdaiwa pia ambae alimuunga mkono jirani kwa kusema kweli
wanachuo hao walikua wezi, wananchi wakakusanyika na kuanza kuwapiga.
Kilichopelekea wananchi kutotoa
nafasi ya kuwasikiliza wanachuo walipojitetea ni pamoja na mfululizo wa
matukio ya uhalifu ambayo yamekua yakitokea kwenye hicho kijiji kwa
siku za karibuni kwa wanakijiji mbalimbali kuibiwa.
Wednesday, October 17, 2012
Home
Unlabelled
HAWA NDIO WAUAJI WA WALE WANACHUO WANNE NIGERIA, WALIWACHOMA MOTO KWA TUHUMA ZA WIZI WAKATI SIO KWELI.
No comments:
Post a Comment