Pages - Menu

Tuesday, October 9, 2012

BUNDESLIGA NEWS: BLASZCZYKOWISKI KUIKOSA REAL MADRID


Klabu ya Borrusia Dortmund itakosa huduma ya kiungo wake  Jakub Blaszczykowski katika Klabu bingwa barani Ulaya juma lijalo dhidi ya Real Madrid  baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mechi ya mwishoni mwa juma nchini Ujerumani.
Taarifa ya mtandao wa klabu hiyo imesema itakosa huduma ya kiungo huyo kufuatia mechi waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Hannover 96.
Pia imesema atakosa mechi ya Poland kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil jumanne itakayofuata.
You might also like:

No comments:

Post a Comment