
.
Ni taarifa ya kuhuzunisha
ambayo niliiweka millardayo.com juzi kuhusu wanachuo wanne wa Nigeria
waliouwawa na wananchi wenye hasira na waliojichukulia sheria mikononi
kwenye kijiji cha Aluu baada ya wanachuo hao kutuhumiwa kuwa wezi na mtu
ambae mmoja wao alikua anamdai pesa.
Baada ya vifo vyao ukweli ndio
umejulikana kwamba wanachuo hao hawakuwa wezi bali walisingiziwa,
kutokana na hilo wanachuo wenzao wenye hasira waliingia mtaani kwenye
kijiji cha Aluu ili kulipa kisasi.

Huyu
mzee wa miaka 65 anasema katika miaka yake yote ya kazi ndio aliweza
kujipatia hizi mali ambazo ndio zimeharibiwa na wanachuo waliolipa
kisasi, hajui ataipeleka wapi familia yake ya watoto 15.
Wamechoma moto nyumba kadhaa,
wamechukua mali za watu wakiwemo wafanyabiashara pamoja na pesa zao na
kufanya uharibifu mwingine na fujo juu ikiwa ni kulipa kisasi kwa
wananchi wa kijiji hicho ambacho hivi karibuni kimekua kikikumbwa na
matukio ya uhalifu ndio maana ilikua rahisi kuamini pia vijana hao wanne
walikua wezi ambapo wakazi wa kijiji cha Aluu walihama makazi yao kwa
kukimbia baada ya kusikia kundi la wanachuo hao likija kwa nguvu.

Hawa ndio wanafunzi wanne waliouwawa kinyama, walivuliwa nguo na kutembezwa uchi kabla ya kuchomwa moto hadharani.

.

.by MillardAyo in News
No comments:
Post a Comment