NEWZ>>>FILEX MMARI
Msanii anayefanya poa hivi sasa na ngoma ya 'Dear God' amesema kuwa toka
atoe wimbo wake wa 'Dear God' amepata maombi mengi kutoka kwa washabiki
wangu wakitaka yeye kutoa album.Kala alisema kuwa kutokana na maombi
hayo ya mashabiki anafikiria kutoa album yake ya kwanza na si kwaajili
ya kufanya biashara bali ni kwaajili ya kuwaridhisha mashabiki
Kala Jeremiah anasema kuwa album hiyo ambayo itakuwa na ngoma zake hata
za kipindi cha nyuma kama 'Wimbo wa Taifa', 'Ningekuwa Raisi' na zingine
nyingi.Alisema kuwa album hiyo ataiuza mwenyewe na itakuwa ni gharama
nafuu ili kila mtu aweze kuipata, "yani kiasi cha pesa ambacho nitakuwa
nauza album hiyo kitakuwa ni kwaajili ya gharama ambazo nimezitumia
kutengeneza album hiyo", Kala.
No comments:
Post a Comment